• HABARI MPYA

  Wednesday, August 09, 2023

  WAGENI WOTE SIMBA, YANGA NA SINGIDA 'WAPIGWA STOP' NGAO YA JAMII  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kwamba ni Azam FC iliyowasilisha vibali vya wachezaji wake 10 wa kigeni kwa ajili ya kucheza michuano ya Ngao ya Jamii inayotarajiwa kuanza leo Jijini Tanga.
  Michuano hiyo ya timu nne inatarajiwa kuanza leo Saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, mabingwa watetezi Yanga wakifungua dimba na Azam FC, wakati kesho  Simba SC itameyana na Singida Fountain Gate.
  Washindi wa mechi hizo mbili leo na kesho watakutana katika Fainali Jumapili katika mchezo ambao utatanguliwa mechi ya kusaka mshindi wa Tatu hapo hapo Mkwakwani. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAGENI WOTE SIMBA, YANGA NA SINGIDA 'WAPIGWA STOP' NGAO YA JAMII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top