• HABARI MPYA

  Monday, August 28, 2023

  KMKM YACHAPWA 3-1 NA KUTUPWA NJE ETHIOPIA LIGI YA MABINGWA


  TIMU ya KMKM ya Zanzibar imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-1 na wenyeji, St George katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali usiku wa Jumapili Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, Ethiopia.
  Mabao ya St George yamefungwa na  viungo Dawit Tefera Alemu dakika ya 49, Natnael Zeleke Tadesse dakika ya 65 na mshambuliaji Abel Yalew Tilahun dakika ya 79, baada ya KMKM kutangulia na bao la mshambuliaji wake, Salum Akida Shukuru dakika ya 24.
  Kwa matokeo hayo, St George wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2 kufuatia kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam na sasa watamenyana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMKM YACHAPWA 3-1 NA KUTUPWA NJE ETHIOPIA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top