• HABARI MPYA

  Sunday, August 13, 2023

  ALLY SALIM SHUJAA SIMBA YABEBA NGAO KWA MATUTA TANGA


  TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya watani, Yanga kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Shujaa wa Simba kwa mara nyingine leo amekuwa kipa Ally Salum aliyeokoa penalti tatu mfululizo za viungo Mganda Khalid Aucho, Pacome Zouzoua na beki Kouassi Attohoula Yao, wote wa Ivory Coast, huku Mburkinabe Stephane Aziz Ki pekee akifunga upande wa Yanga.
  Waliofunga penalti za Simba ni kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Muzamil Yassin na washambuliaji Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana na Mkongo, Jean Othos Baleke huku Mrundi Saido Ntibanzokiza iliokolewa na kipa Mmali, Djigui Diarra na ya Mzambia, Moses Phiri ikienda juu ya lango.
  Simba ilifika Fainali kwa ushindi wa penalti pia 4-2 dhidi ya Singida Fountain Gate Alhamisi huku Yanga wakiifunga Azam FC 2-0 Jumatano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLY SALIM SHUJAA SIMBA YABEBA NGAO KWA MATUTA TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top