• HABARI MPYA

  Sunday, August 06, 2023

  ARSENAL WAITWANGA MAN CITY KWA MATUTA MECHI YA NGAO


  TIMU ya Arsenal imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Manchester City kufuatia sare ya 1-1 leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Kiungo chipukizi wa England, Cole Jermaine Palmer alianza kuifungia Manchester City dakika ya 77, kabla ya mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard kuisawazishia Arsenal dakika ya 90 na ushei.
  Na katika mikwaju ya penalti, Mreno Bernardo Silva pekee aliifungia Manchester City huku  Mbelgiji Kevin De Bruyne na Mspaniola Rodrigo Hernández Cascante ‘Rodri’ wakikosa katika tatu za mwanzo.
  Na waliofunga penalti za Arsenal mfululizo ni Mnorway Martin Odegaard, Trossard, Muingereza Bukayo Saka na Mreno Fábio Vieira.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL WAITWANGA MAN CITY KWA MATUTA MECHI YA NGAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top