• HABARI MPYA

  Tuesday, April 04, 2023

  MTINE AENEA MISRI KUIWAKILISHA YANGA DROO YA CAF


  AFISA Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andre Mtine ameondoka nchini jioni hii kuelekea Jijini Cairo nchini Misri kuiwakilisha klabu yake kwenye droo ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Baada ya kuongoza Kundi D mbele ya US Monastirienne ya Tunisia itapangiwa mmoja kati ya washindi wa pili wa Kundi A, B na C ambao ni USM Alger ya Algeria, Rivers United ya Nigeria na Pyramids ya Misri.
  Monastirienne iliyomaliza ya pili Kundi D itapakutana na mmoja wa vinara wa makundi A, B na C ambao ni Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na FAR Rabat ya Morocco.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTINE AENEA MISRI KUIWAKILISHA YANGA DROO YA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top