• HABARI MPYA

  Tuesday, April 04, 2023

  FOUNTAIN GATE YAPANGWA KUNDI A MICHUANO YA CAF  TIMU ya wasichana ya Tanzania, Fountain Gate Secondary School ya Dodoma imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Edendale Technical School na Scan Aid ya Gambia katika michuano ya shule za sekondari ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), maarufu kama African Schools Football Championship.
  Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanz a leo Uwanja wa the King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini hadi Aprili 8, Kundi B linaundwa na timu za CEG Mfilou ya Kongo, Anse Boileau ya Shelisheli, CEG Colby ya Benin na Ecole Omar IBN Khatab ya Morocco.
  Upande wa wavulana Kundi A kuna Clapham High School (South Africa), CS Horizon of Bukavu (DRC) na CEM Belaouche Mouhend Oulhadji (Algeria), wakati Kundi B kuna Salima Secondary School (Malawi), Complexe Scolaire Ben Sekou Sylla (Guinea), CEG Sainte Rita (Benin) na Royal Giants High School (Uganda).
  Taasisi ya Motsepe Foundation, inayomilikiwa n Rais wa CAF imechangia dola za Kimarekani Milioni 10 kwenye michuano hiyo na kuifanya iwe ya kitajiri Zaidi miongoni mwa michezo ya wanafunzi barani. 
  Mshindi kwa upande wa wasichana na wavulana atazawadiwa USD 300,000 kila mmoja na washindi wa pili watapata USD 200,000 wakati wa tatu atapata USD 150,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAPANGWA KUNDI A MICHUANO YA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top