• HABARI MPYA

  Saturday, April 08, 2023

  AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo, Mnigeria Isah Aliyu Ndala dakika ya 39 na mzawa, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 60, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Onesmo Mayaya dakika ya 75.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 50, ingawa inabaki nafasi ya nne, ikizidiwa pointi moja na Singida Big Stars baada ya wote kucheza mechi 26.
  Mtibwa Sugar bao kwa upande wao baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 29 za mechi 26 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top