• HABARI MPYA

  Friday, April 07, 2023

  BALEKE APIGA HAT TRICK SIMBA YAITANDIKA IHEFU 5-1 ASFC


  VIGOGO, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Ihefu SC ya Mbeya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Baleke matatu dakika za pili, 16 na 28 na viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 40 na Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Ihefu SC limefungwa na kiungo pia Raphael Daudi Lothi dakika ya 61.
  Sasa Simba SC itakutana na Azam FC katika mchezo wa Nusu wa Fainali. Ikumbukwe Azam FC ilitangulia Nne Bora Jumatatu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar hapo hapo Chamazi.
  Timu nyingine ambayo tayari ipo Nusu Fainali na Singida Big Stars iliyoitoa Mbeya City kwa kuichapa 4-1 na yenyewe itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho kesho kati ya mabingwa watetezi, Yanga na Geita Gold.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALEKE APIGA HAT TRICK SIMBA YAITANDIKA IHEFU 5-1 ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top