• HABARI MPYA

  Wednesday, July 06, 2022

  MTIBWA SUGAR YAFANIKIWA KUBAKI KIGI KUU


  TIMU ya Mtibwa Sugar Imefanikiwa kubaki katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara licha ya kuchapwa 1-0 na Tanzania Prisons katika mchezo wa marudiano ya mchujo wa kubaki kwenye ligi hiyo jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Mudathir Abdallah dakika ya 53 na Mtibwa inabaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla 3-2 kufuatia kushinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Sasa Prisons itamenyana na JKT Tanzania kutoka Championship, mechi ya kwanza ya Jumamosi Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na marudiano Jumatano ijayo Uwanja wa Sokoine.
  Mshindi atacheza tena Ligi Kuu msimu ujao, wakati timu itakayofungwa itashiriki Championship.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAFANIKIWA KUBAKI KIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top