• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2022

  SIMBA YAICHAPA NAMUNGO 5-0 LIGI YA VIJANA U20

  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kundi A Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Shujaa wa Simba B inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani Mussa Hassan Mgosi ni Michael Joseph aliyefunga mabao matatu, moja kwa kwa penalti huku mengine yakifungwa na Joseph Mbaga na Rahim Shomari.
  Mechi nyingine ya Kundi A leo, Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Biashara United hapo hapo Chamazi.
  Mechi za Kundi C, Azam FC iliichapa Tanzania Prisons 3-1 na Coastal Union ikaitandika Mbeya City 4-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAICHAPA NAMUNGO 5-0 LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top