• HABARI MPYA

  Tuesday, July 19, 2022

  AZAM FC YAKAMILISHA USAJILI NA BEKI MSENEGAL


  KLABU ya Azam FC imefunga usajili wake kwa kumtambulisha beki wa kati, Malickou Ndoye mwenye umri wa miaka 22 kutoka Teungueth ya kwao, Senegal.
  Ndoye anafanya jumla ya wachezaji tisa wapya, wengine kipa mkongwe Mcomoro mzaliwa wa Ufaransa, Ali Ahamada na viungo, Mghana James, Kipre Junior, Tape Edinho kutoka Ivory Coast, Mnigeria, Isah Ndala.
  Wengine ni wazawa, beki wa kulia, Nathaniel Chilambo kutoka Ruvu Shooting, viungo washambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union na Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji na kikosi kinaanza mazoezi leo jioni Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAKAMILISHA USAJILI NA BEKI MSENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top