• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2022

  HERSI APITISHWA BILA KUPINGWA KUWA RAIS YANGA


  MHANDISI Hersi Ally Said amepitishwa bila kupingwa na wanachama kuwa Rais wa klabu ya Yanga katika uchaguzi Mkuu unaofanyika leo ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Wakili Malangwe Ally Mchungahela alitumia kanuni ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoelekeza mgombea wa Urais anapokuwa peke yake apitishiwe au kupingwa bila kupigiwa kura.
  Kwa sasa uchaguzi wa nafasi tano za Ujumbe na Makamu wa Rais ndio unaendelea ukumbini hapo.
  Mchuano mkali upo katika nafasi ya Makamu wa Rais ambapo wagombea Arafat Haji na mwanamama Suma Mwaitenda wamepitishwa kuwania nafasi hiyo.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HERSI APITISHWA BILA KUPINGWA KUWA RAIS YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top