• HABARI MPYA

  Thursday, July 14, 2022

  SIMBA SC YAENDA KUWEKA KAMBI MISRI


  KIKOSI cha Simba kimeondoka leo jioni nchini kwenda mjini Ismailia nchini Misri kuweka kambi ya kujiansaa na msimu mpya.
  Simba imeondoka na wachezaji wake wote, wakiwemo wapya, wazawa wawili, kiungo Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza iliyoshuka Daraja.
  Wengine ni wageni kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union, winga Mghana, Augustine Okrah kutoka Asante Kotoko ya kwao na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao. Kikosi hicho chini ya kocha mpya, Mserbia Zoran Manojilovic ‘Maki’ kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 5 kwa ajili ta Tamasha lake la Simba Day siku tatu baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDA KUWEKA KAMBI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top