• HABARI MPYA

  Monday, July 11, 2022

  AZAM FC YAAJIRI KOCHA MWINGINE MSPANIOLA, NI MIKEL GUILLEN


  KLABU ya Azam FC imemuajiri Mspaniola, Mikel Guillen kuwa Kocha mpya wa mazoezi ya viungo.
  Taarifa ya Azam FC imesema Guillen ni kocha wa viwango vya juu, mwenye uzoefu wa kufundisha timu za Aris Limassol ya Cyprus, inayoshiriki Ligi ya Conference European Cup,  Bengaluru ya India na Dinamo Bucuresti ya Romania.
  Azam imesema uzoefu wake umemfanya kufundisha baadhi ya wachezaji wakubwa, akiwemo Sunil Chhetri, mfungaji namba sita wa mabao duniani kwa upande wa timu za Taifa.
  Wengine aliowanoa ni Gordon Schildenfeld, aliyecheza fainali za Kombe la Dunia na Euro akiwa na Taifa lake la Croatia na Manu Garcia, aliyewahi kuwa nahodha wa Alaves kwa zaidi ya mechi 100 kwenye La Liga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAAJIRI KOCHA MWINGINE MSPANIOLA, NI MIKEL GUILLEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top