• HABARI MPYA

  Friday, July 08, 2022

  BANGALA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU, MAYELE BAO BORA LA MSIMU


  KIUNGO mlinzi wa Yanga, Yanick Litombo Bangala raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ndiye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2021-2022. 
  Bangala ameshinda tuzo hiyo usiku wa jana Jijini Dar es Salaam akiwaangusha Wakongo wenzake, beki Henock Inonga Baka wa Simba na mshambuliaji Fiston Kalala Mayele wa Yanga pia.
  Bangala pia ameshinda Tuzo ya Kiungo Bora, huku Inonga akishinda Tuzo ya Beki Bora na Mayele akafanikiwa kuondoka na Tuzo ya Bao Bora la Msimu alilofunga kwa tik tak dhidi ya Biashara United.
  Djigui Diarra wa Yanga ndiye Kipa Bora wa msimu baada ya nyota huyo kutoka Mali kuwashinda Aishi Manula wa Simba na wa Geita Gold, wakati Dickson Mhilu amekuwa Mchezaji Bora Chipukizi.
  Mfungaji wa Ligi Kuu, George Mpole wa Geita Gold na Mfungaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Abdul Suleiman 'Sopu' wa Coastal Union pia walipewa tuzo zao. 
  Sopu pia ambaye amekwishasaini Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, pia ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa ASFC, huku Kipa wa michuano hiyo pia akitoka Coastal, Mohamed Mohamed.
  Mchezaji Bora wa Ligi ya Wanawake ni Fatma Issa 'Densa' na Refa Bora ni Ahmed Arajiga wa Manyara. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BANGALA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU, MAYELE BAO BORA LA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top