• HABARI MPYA

  Wednesday, July 13, 2022

  SIMBA NA YANGA ZATUPWA NJE LIGI YA VIJANA U20


  TIMU za vijana za Simba na Yanga zote zimetolewa katika Robo Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 leo Uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Ilianza Coastal Union kuitupa nje Simba SC kwa kuilaza 1-0, bao pekee la Mgaya Khamis dakika ya 48.
  Ikifuatia Mbeya Kwanza kuitoa Yanga kwa kuichapa 1-0 pia, bao pekee la Ahmed Hassan dakika ya 51.
  Mechi nyingine za Robo Fainali, wenyeji, Azam FC walikwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1.
  Katika mchezo wa kwanza, mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar waliitupa nje Geita Gold kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1.
  Nusu Fainali ni Ijumaa, Mbeya Kwanza na Coastal Union na Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar hapo hapo Azam Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZATUPWA NJE LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top