• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2022

  SIMBA SC YAANZA KUTAMBULISHA WAPYA NA KYOMBO


  VIGOGO, Simba SC wametambulisha mchezaji wa pili mpya kuelekea msimu ujao, ambaye ni mshambuliaji Habib Haji Kyombo kutoka Mbeya Kwanza iliyoshuka Daraja.
  Awali, Kyombo alitambulishwa Singida Big Stars mwezi uliopita baada tu ya dirisha la usajili kufunguliwa, lakini baadaye klabu hiyo ikatangaza kuachana naye.
  Mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri ndiye mchezaji mpya wa kwanza kutambulishwa Simba akitokea Zanaco ya kwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAANZA KUTAMBULISHA WAPYA NA KYOMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top