• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2022

  HERSI AMTAMBULISHA NYOTA WA ZAMANI WA NEWCASTLE


  RAIS mpya wa klabu ya Yanga, Mhandsi Hersi Ally Said amemtambulisha kiungo wa kimataifa wa Burundi, Gael Bigirimana kuwa mchezaji mpya wa tatu wa klabu hiyo kuelekea msimu msimu ujao.
  Bigirimana anayetokea klabu ya Glentoran ya Ligi Kuu ya 
  Ireland Kaskazini anawafuatia mshambuliaji Mzambia, Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na winga Mghana, Bernard Morrison kutoka Simba SC waliotambulishwa awali.
  Bigirimana mwenye umri wa umri wa miaka 38, mzaliwa wa Bujumbura, aliibukia timu ya vijana ya Coventry City ya England mwaka 2005 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2011 ambako alicheza mechi 26.
  Mwak 2012 akahamia Newcastle United ambako baada ya kufunga bao moja katika mechi 13, akatolewa kwa mkopo Rangers ya Scotland mwaka 2015 na msimu wa 2015–2016 akarejea Coventry City kwa mkopo ambako mwisho wa msimu alinunuliwa moja kwa moja na kucheza jumla ya mechi 33 hadi 2017 alipohamia Motherwell ya Scotland ambako alicheza mechi 46 na kufunga mabao mawili.
  Mwaka 2019 akahamia Hibernian ya Scotland ambako alicheza mechi moja tu kabla ya kuhamia Solihull Moors ya Daraja la Tano England mwaka 2019 na mwaka 2020 ndipo alipotua Glentoran ambako baada ya mechi 43 mwaka huu anajiunga na Yanga.
  Tangu mwaka 2015 ameichezea timu ya taifa ya Burundi, Int'hamba Murugamba jumla ya mechi 16. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HERSI AMTAMBULISHA NYOTA WA ZAMANI WA NEWCASTLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top