• HABARI MPYA

  Sunday, July 24, 2022

  MSUVA AJIUNGA NA AL-QADSIYAH YA SAUDI ARABIA

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Saimon Happygod Msuva amejiunga na klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabian baada ya kuachana na Wydad Athletic ya Morocco.
  Msuva anatua Al-Qadsiah yenye maskani yake mji wa Khobar inayotumia Uwanja wa Prince Saud bin Jalawi, baada ya kuichezea Wydad tangu mwaka 2020 akitokea timu nyingine ya Morocco, Difaâ El Jadida aliyojiunga nayo mwaka 2017.
  Alikwenda Morocco moja kwa moja mwaka 2020 akitokea nyumbani, Tanzania, klabu ya Yanga aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Moro United, iliyomchukua Azam FC mwaka 2010.


  Anakuwa mmoja wa wachezaji watano wa kigeni Al-Qadsiah, wengine beki Mserbia, Uroš Vitas, viungo Ibrahim Amada kutoka Madagascar, Moha Rharsalla wa Morocco na washambuliaji Mrundi, Cedric Amissi na Mzambia Walter Bwalya anayecheza kwa mkopo kutoka Al-Ahly ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AJIUNGA NA AL-QADSIYAH YA SAUDI ARABIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top