• HABARI MPYA

    Friday, July 08, 2022

    AZAM FC YAACHA MCHEZAJI WA TATU, NI NICO WADADA


    KLABU ya Azam FC imetangaza kuachana na beki wetu wa kulia, Mganda, Nickolas Wakiro Wadada baada ya miaka mitatu ya kuwa na timu hiyo.
    Taarifa ya Azam FC imesema kwamba Wadada anaondoka baada ya kumaliza rasmi mkataba wake na msimu wake mzuri zaidi ni 2019-2020 aliposhinda tuzo ya Beki Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
    Anakuwa mchezaji wa tatu kuachwa baada ya Mganda mwenzake, kipa Mathias Kigonya na beki Mcameroon, Yvan Mballa.
    Tayari Azam FC imemsajili wachezaji wapya sita ambao ni wazawa beki wa kulia, Nathaniel Chilambo kutoka Ruvu Shooting, viungo washambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ kutoka Coastal Union na Cleophace Mkandala kutoka Dodoma Jiji.
    Wengine ni viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala - usajili wa safari hii ukifanywa na mmiliki wa timu mwenyewe, Yussuf Bakhresa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdukkarim Amin ‘Popat’.
    Azam FC imeimarisha benchi la ufundi kwa kumrejesha aliyewaji kuwa mchezaji na kocha wake Msaidizi, Kali Ongala safari hii akipewa jukumu la kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, yaani feetness coach.
    Aidha, pia imemuajiri kocha mpya wa makipa, Mspaniola, Dani Cadena ambaye amewahi kufundisha klabu za Sevilla na Real Betis za Hispania na nyingine za China na Asaudi Arabia akiwa na uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAACHA MCHEZAJI WA TATU, NI NICO WADADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top