• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2022

  BI HINDU MWIGIZAJI MKONGWE MWANA SIMBA AFARIKI DUNIA


  MWANACHAMA mkongwe wa Simba SC, Chuma Suleiman maarufu kama Bi. Hindu amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjukuu wake, Bi. Hindu aliyekuwa mwigizaji maarufu wa filamu na tamthiliya nchini, amekutwa na umauti baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda.
  Klabu ya Simba imetoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo na kwamba wapo pamoja na familia katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
  Mazishi yatafanyika kesho Jumapili saa 7 mchana eneo la Magomeni Mapipa katika makaburi ya Mwinyimkuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BI HINDU MWIGIZAJI MKONGWE MWANA SIMBA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top