• HABARI MPYA

    Tuesday, July 05, 2022

    RAIS SAMIA ATOA VIFAA KOMBE LA YAMLEYAMLE

    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa, Samia Suluhu Hassan ametoa vifaa vya michezo kwa timu zote 45 zinazoshiriki mashindano ya kombe la Yamleyamle Zanzibar ili timu ziweze kufanya vizuri hatimaye  kuwapata wachezaji bora na wenye  vipaji ambao wataunganishwa  kwenye timu ya Taifa.
    Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Julai 3, 2022 wakati akizindua mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar ambapo amesema Mhe. Rais ametoa mipira 45 kwa ajili ya timu hizo na jezi.
    “Niwaombe  tunapojipanga kwenda kuandaa mashindano ya AFCON,  tuleteeni orodha  ya  vijana wanaofanya vizuri tutahakikisha tunawaingiza kwenye time zetu za taifa, tutawaendeleza, tutakuza vipaji vyao kwa maslahi  ya Serikali zote mbili SMT na SMZ”. Amesisitiza Mhe, Mchengerwa.


    Amewapongeza kwa kuandaa mashindano hayo ambapo amefafanua kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaandaa mashindano ya AFCON  2027 na kusisitiza kuwa inawezekana iwapo kila  mdau atachukua wajibu wake.
    Aidha, amefafanua kuwa eneo la soka ndilo eneo pekee ambalo  linaweza  kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi ya dini zao, rangi wala  makabila yao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS SAMIA ATOA VIFAA KOMBE LA YAMLEYAMLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top