• HABARI MPYA

  Monday, July 11, 2022

  YANGA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA VIJANA


  TIMU ya Yanga imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 4-3 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Kundi D jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na Clement Mzinza mawili, Mashoto na Juventus, wakati ya Kagera yamefungwa na Kihulo, Nasri aliyejifunga na Feisal Nassor.
  Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza nafasi ya kwanza kwenye Kundi lao baada ya kukusanya pointi sita, wakifuatiwa na Geita Gold iliyoizidi wastani wa mabao KMC iliyomaliza nafasi ya tatu, huku Kagera Sugar iliyokusanya pointi mbili ikishika mkia.
  Mechi nyingine za jana ni za Kundi B zilizomalizika kwa sare zote, Ruvu Shooting 2-2 Dodoma Jiji na Mbeya Kwanza 1-1 Mtibwa Sugar hapo hapo Chamazi.
  Timu nyingine zilizotinga Robo Fainali ni Simba na Polisi Tanzania kutoka Kundi A, Mtibwa Sugar na Mbeya Kwanza Kundi B na Azam FC na Coastal Union Kundi C.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top