• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2022

  YANGA YAENDELEZA HISANI KABLA YA MECHI ZAKE


  KLABU ya Yanga imeendeleza utamaduni wa kufanya shughuli za Kijamii kabla ya mechi zake baada ya leo kutembelea kituo cha kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kiitwacho Njiro Recovery Sober House Jijini Arusha.
  Katika ziara hiyo, Yanga ambayo kesho itamenyana na Coastal Union ya Tanga katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), imeongozana na Mkuu wa Wilaya Arusha Mjini Said, Mohamed Mtanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDELEZA HISANI KABLA YA MECHI ZAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top