• HABARI MPYA

  Tuesday, July 12, 2022

  SIMBA KUWEKA KAMBI MISRI, ITAONDOKA ALHAMISI DAR


  KLABU ya Simba inatarajiwa kuondoka keshokutwa nchini kwenda kuweka kambi Misri kujiandaa na msimu ujao.
  Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kwamba  amesema kikosi kitaondoka na wachezaji wote waliosajiliwa, kasoro wale watakaokuwa kwenye timu zao za taifa.
  "Timu yetu itaondoka tarehe 14 mwezi huu kwenda kwenye mji wa Ismailia nchini Misri na itarudi Agosti 5. Tutaondoka na wachezaji wote isipokuwa wale ambao watakuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa. Tukirejea itakuwa ni Simba Day." amesema.
  Katika mkutano huo, Simba pia imemtambulisha kocha wake mpya, Zoran Manojilovic ‘Maki’ ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mmoja akifanya vizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA KUWEKA KAMBI MISRI, ITAONDOKA ALHAMISI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top