• HABARI MPYA

  Wednesday, July 13, 2022

  WINGA MGHANA, OKRAH AJIUNGA NA SIMBA SC

  KLABU ya Simba imemtambulisha winga Mghana, Augustine Okrah kutoka klabu ya Asante Kotoko ya kwao.
  Okrah aliibukia timu za vijana za Bechem United na Red Bull za kwao, Ghana kabl ya kusajiliwa na Asante Kotoko mwaka 2012, ambayo mwaka 2013 ilimpeleka kwa mkopo Liberty Professionals ambako baada ya miezi kadhaa akahamia Bechem United hadi mwaka 2014 alipojiunga na BK Hacken ya Sweden.
  Mwaka 2015 alijiunga na El - Merreikh kabla ya 2016 kuhamia El - Hilal ya Sudan hadi 2018 NorthEast United, zote za Sudan na mwaka 2019 akarejea Asante Kotoko hadi sasa anajiunga na Simba.
  Amecheza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2013 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2019.
  Okrah anakuwa mchezaji mpya wa tano Simba baada ya beki, Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar, mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza iliyoshuka Daraja, kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao.
  Kikosi cha Simba inatarajiwa kuondoka kesho nchini kwenda kuweka kambi mjini Ismailia nchini Misri hadi Agosti 5 kitakaporejea kwa ajili ta Tamasha lake la Simba siku tatu baadaye.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WINGA MGHANA, OKRAH AJIUNGA NA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top