• HABARI MPYA

  Sunday, July 10, 2022

  ARAFAT NDIYE MAKAMU WA RAIS YANGA SC, WAJUMBE...


  MSHINDI wa nafasi ya MAKAMU wa Rais wa klabu ya Yanga ni Arafat Haji baada ya kupata kura 545 dhidi ya kura 234 mpinzani wake Suma Mwaitenda katika uchaguzi uliofanyika jana ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Malangwe Ally Mchungahela, waliopiga kura walikuwa 785 na kura zilizoharibika zilikuwa ni sita (6). 
  Wajumbe watano waliochaguliwa kuunda Kamati ya Utendaji kati ya 17 waliogombea ni pamoja na Alexander Ngai, Munir Said, Rodgers Gumbo, Seif Gulamali na Everlist Yanga Makaga.
  Mapema uchaguzi huo ulipoanza tu, Mhandisi Hersi Ally Said aliitishwa bila kupingwa na wanachama kuwa Rais wa klabu ya Yanga.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Wakili Malangwe Ally Mchungahela alitumia kanuni ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoelekeza mgombea wa Urais anapokuwa peke yake apitishiwe au kupingwa bila kupigiwa kura.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARAFAT NDIYE MAKAMU WA RAIS YANGA SC, WAJUMBE... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top