• HABARI MPYA

  Sunday, July 03, 2022

  AZAM FC YAMTEMA KIGONYA, YAMREJESHA KALI ONGALA


  KLABU ya Azam FC imeachana na kipa wake, Mganda 
  Mathias Kigonya baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
  Mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, Kigonya alikuwa amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake na akatuomba anataka kuondoka kutafuta changamoto sehemu nyingine na tukafikia makubaliano ya kuachana.
  "Tunapenda kumshukuru Kigonya, kwa mchango wake alioutoa kwenye klabu yetu kwa kipindi chote tokea alipojiunga nasi Januari mwaka jana, akitokea Forest Rangers ya Zambia," imesema taarifa ya Azam FC.


  Aidha, Azam FC imemrejesha aliyewaji kuwa mchezaji na kocha wake Msaidizi, Kali Ongala safari hii akipewa jukumu la kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, yaani feetness coach.
  Azam FC tayari imesajili wachezaji wapya wanne ambao ni kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala, kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Dodoma Jiji, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.
  Azam FC imeimarisha benchi la ufundi kwa KI muajiri kocha mpya wa makipaMspaniola, Dani Cadena ambaye amewahi kufundisha klabu za Sevilla na Real Betis za Hispania na nyingine za China na Asaudi Arabia akiwa na uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.
  Usajili wa safari hii Azam FC unafanya na mmiliki wa timu, Yussuf Bakhresa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdukkarim Amin ‘Popat’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMTEMA KIGONYA, YAMREJESHA KALI ONGALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top