• HABARI MPYA

    Friday, July 22, 2022

    PAPE SAKHO ASHINDA TUZO YA BAO BORA AFRIKA 2022

    BAO la kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho alilofunga dhidi ya ASEC kwenye mechi ya Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika limeshinda Tuzo ya Bora la Mwaka.
    Katika sherehe za utoaji wa Tuzo hizo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa Alhamisi mjini Rabat nchini Morocco, Sakho ameshinda dhidi ya Gabadinho Mhango wa Malawi na Orlando Pirates na Zouhair El Moutaraji wa Morocco na Wydad Athletic alioingia nao Fainali.
    Sakho alifunga bao hilo dakika ya 12 tu akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe katika ushindi wa 3-1 dhidi ASEC Mimosas  ya Februari 13, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mabao mengine ya Simba siku hiyo yalifungwa na Kapombe dakika ya 79 na winga Mmalawi, Peter Banda dakika ya 81 akimalizia pasi ya Nahodha, John Bocco, wkaati bao pekee la ASEC lilifungwa na Stephane Aziz Ki 60 dakika ya 60.Senegal & Simba)
    Washindi wengine wa tuzo za CAF mwaka huu ni nyota wa Senegal aliyejiunga na Bayern Munich akitokea Liverpool, Sadio Mane ambaye amebeba tena Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mbele ya mwananchi mwenzake, kipa Edouard Mendy wa Chelsea na Mohamed Salah wa Misri na Liverpool.
    Ulikuwa usiku mzuri, baada ya Wasenegal wengine kubeba tuzo, Aliou Cisse akichukuwa ya Kocha Bora wa Mwaka na Pape Matar Sarr wa Tottenham Hotspur akiondoka na ya Mwanasoka Bora Chipukizi.
    Asisat Oshoala wa Nigeria ameshinda kwa mara ya tano ya rekodi Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike, huku Senegal ikishinda tuzo ya timu Bora ya Taifa na Wydad Athletic ikibeba Tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume na Mamelodi Sundowns Klabu Bora ya Wanawake.
    WASHINDI WOTE TUZO ZA CAF
    BAO BORA LA MWAKA
    Pape Ousmane Sakho (Senegal & Simba)
    MWANASOKA BORA WA MWAKA WA KIUME
    Sadio Mane (Senegal and Bayern Munich)
    MWANASOKA BORA WA KIKE
    Asisat Oshoala (Nigeria and FC Barcelona)
    MCHEZAJI BORA WA KIKE WA KLABU
    Evelyn Badu (Ghana & Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)
    MCHEZAJI BORA WA KIUME WA KLABU
    Mohamed El Shenawy (Egypt & Al Ahly)
    MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIKE
    Evelyn Badu (Ghana & Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)
    MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIUME
    Pape Matar Sarr (Senegal and Tottenham Hotspur)
    KOCHA BORA WA MWAKA MWANAMKE
    Desiree Ellis (Afrika Kusini)
    KOCHA BORA WA MWAKA MWANAUME
    Aliou Cisse (Senegal)
    KLABU BORA YA MWAKA YA WANAWAKE
    Mamelodi Sundowns (South Africa)
    KLABU BORA YA MWAKA YA WANAUME
    Wydad Athletic Club (Morocco)
    TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME
    Senegal
    TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME
    Itapatikana baada ya Fainali ya Afrika za Wanawake zinazoendelea Morocco
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAPE SAKHO ASHINDA TUZO YA BAO BORA AFRIKA 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top