• HABARI MPYA

  Sunday, July 03, 2022

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA PRISONS 3-1 PALE PALE SOKOINE


  TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mechi ya kwanza ya mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Jaffar Kibaya mawili, dakika ya 22 na 55 na Salum Kanoni dakika ya 71, wakati bao pekee la Prisons limefungwa na Marco Mhilu dakika ya 60.
  Timu hizo zitarudiana Jumatano Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na JKT Tanzania kutoka Championship.
  Mshindi ndiye atacheza tena Ligi Kuu msimu ujao – na mechi dhidi ya JKT Tanzania zimepngwa kucheza Julai 9 Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na marudiano Julai 13 Sokoine au Manungu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA PRISONS 3-1 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top