• HABARI MPYA

  Sunday, July 17, 2022

  NI MTIBWA SUGAR MABINGWA TENA LIGI YA VIJANA U20


  TIMU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuwafunga Mbeya Kwanza mabao 4-1 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ezekiel Eusebio dakika ya 29, Ladack Chasambi dakika ya 45, Said Mkopi dakika ya 84 na Omary Suleiman dakika ya 90 na ushei, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Willie Thobias dakika ya 68.
  Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, Azam FC imeifunga Coastal Union kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 hapo hapo Chamazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MTIBWA SUGAR MABINGWA TENA LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top