• HABARI MPYA

  Saturday, July 30, 2022

  TAIFA STARS YASONGA MBELE KUFUZU CHAN


  TANZANIA imesonga mbele katika kuwania tiketi ya Fainali za CHAN mwakani baada ya ushindi wa 2-1 leo dhidi ya Somalia Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Abdul Sopu dakika ya 34 na Dickson Job kwa penalti dakika ya 64, wakati la Somalia limefungwa na Farhan Ahmed dakika ya 47.
  Taifa Stars inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YASONGA MBELE KUFUZU CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top