• HABARI MPYA

  Saturday, July 23, 2022

  TAIFA STARS YAICHAPA SOMALIA 1-0 KUFUZU CHAN


  BAO pekee la kiungo mshambuliaji mpya wa Azam FC, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ limeipa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Sopu aliyeng'ara akiwa na Coastal Union ya Tanga misimu mitatu iliyopita baada ya awali kuchezea Ndanda FC ya Mtwara na Simba ya Dar es Salaam, alifunga bao hilo dakika ya 46 akimalizia krosi ya beki wa Yanga, Kibwana Shomari kutoka kulia.
  Timu hizo zitarudiana Jumamosi ijayo Uwanja wa Mkapa, Tanzania wakiwa wenyeji kwenye mbio hizo za CHAN ya mwakani Algeria.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAICHAPA SOMALIA 1-0 KUFUZU CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top