• HABARI MPYA

  Friday, July 15, 2022

  FAINALI LIGI YA VIJANA U20 NI MTIBWA NA MBEYA KWANZA


  FAINALI ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 itazikutanisha Mbeya Kwanza ya Mbeya na Mtibwa Sugar ya Morogoro Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Hiyo ni baada ya timu hizi kuzitupa nje, Azam na Coastal Union katika mechi za Nusu Fainali leo hapo hapo Azam Complex.
  Ilianza Mbeya Kwanza kuitupa nje Coastal Union kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Joel Mwambungu dakika ya 83.
  Ikifuatia Mtibwa Sugar kuitoa Azam kwa penalti 9-8 baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FAINALI LIGI YA VIJANA U20 NI MTIBWA NA MBEYA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top