• HABARI MPYA

  Sunday, July 17, 2022

  SAKHO AINGIZWA BAO LA MWAKA TUZO ZA CAF

  BAO la winga Msenegal wa Simba, Pape Ousmane Sakho alilofunga dhidi ya ASEC kwenye mechi ya Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika limeingia kwenye kipengele cha kuwania Bao Bora la Mwaka Afrika katika Tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
  Sakho alifunga bao hilo dakika ya 12 tu akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe katika ushindi wa 3-1 dhidi ASEC Mimosas  ya Februari 13, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao mengine ya Simba siku hiyo yalifungwa na Kapombe dakika ya 79 na winga Mmalawi, Peter Banda dakika ya 81 akimalizia pasi ya Nahodha, John Bocco, wkaati bao pekee la ASEC lilifungwa na Stephane Aziz Ki 60 dakika ya 60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKHO AINGIZWA BAO LA MWAKA TUZO ZA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top