• HABARI MPYA

  Sunday, July 17, 2022

  SIMBA NAYO YAAJIRI KOCHA MTUNISIA


  KLABU ya Simba imemtambulisha Mtunisia, Sbai Karim kuwa Kocha wa Viungo pamoja na Kocha Msaidizi sambamba na mzawa, Suleiman Matola.
  Kwa pamoja, Sbai na Matola watakuwa na jukumu la kumsaidia Kocha Mkuu, Zoran Maki kwenye kutimiza majukumu yake ipasavyo.
  Sbai na Kocha Zoran wanafahamiana vizuri  kwani wamefanya kazi pamoja katika Timu za Wydad Casablanca (Morocco), CR Belouzdad (Algeria) Al Hilal (Sudan) na Al Tai (Saudi Arabia) akiwa msaidizi wake.
  Sbai ni kocha msomi mwenye leseni ya Daraja A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
  Sbai ameifundisha Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kuanzia 2017 mpaka 2020 na kufanikiwa kuchukua mataji makubwa ya Afrika.
  Msimu wa 2018/19 alicheza mchezo wa CAF Super Cup lakini timu yake ya Wydad ilipoteza mechi.
  Msimu wa  2020/2021 alikuwa akiitumikia klabu ya Al Hilal ya Sudan.
  Uongozi wa klabu umezingatia uhusiano chanya uliopo baina ya Kocha Zoran na Sbai ambapo tunaamini kufahamiana kwao kutarahisisha muunganiko wa haraka kikosini kuelekea msimu mpya wa ligi.
  Anakuwa Mtunisia wa pili katika ligi ya Tanzania baada ya Nasrdedine Nabi, kocha Mkuu wa Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NAYO YAAJIRI KOCHA MTUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top