• HABARI MPYA

  Monday, July 04, 2022

  RONALDO AOMBA KURUHUSIWA KUONDOKA MAN UNITED


  MSHAMBULAJI 
  Cristiano Ronaldo ameomba kuruhusiwa kuondoka Manchester United kama itatokea ofa dirisha hili la usajili.
  Taarifa zinasema Mreno huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa anataka kucheza Champions League tena msimu ujao.
  Ronaldo ndiye mfungaji Bora wa Man United msimu uliomalizika kutokana kupachika nyavuni mabao 24, lakiki Mashetani hao Wekundu wakamaliza nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu ya England.
  Ronaldo alirejea Old Trafford msimu uliopita akitokea  Juventus na amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa Man United.
  Na inafahamika klabu za Chelsea y England pia, Bayern Munich ya Ujerumani na Napoli ya Italia zinamuhitaji mkali huyo wa mabao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AOMBA KURUHUSIWA KUONDOKA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top