• HABARI MPYA

  Saturday, July 02, 2022

  AZAM FC YASAJILI KIUNGO FUNDI WA DODOMA JIJI


  KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala, kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Dodoma Jiji.
  Kiungo huyo aliyefanya vizuri msimu uliopita, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
  Mkandala, 21, ni mmoja wachezaji vijana wanaochipukia vizuri, amesaini mkataba huo wenye kipengele cha kuongeza ndani ya miezi sita na hiyo itatokana na kiwango atakachokionyesha.
  Aidha mbali na kuicheza Dodoma Jiji, Mkandala pia amewahi kucheza kwa misimu mitatu ndani ya kikosi cha maafande wa Tanzania Prisons, 2018-2019 hadi 2020-2021.
  Huo unakuwa usajili wa kwanza kwa mchezaji mzawa kuelekea msimu ujao na wa nne kwa ujumla baada ya viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho kutoka Ivory Coast na kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI KIUNGO FUNDI WA DODOMA JIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top