• HABARI MPYA

  Friday, July 22, 2022

  SIMBA YAMTAMBULISHA BEKI WA KATI MUIVORY COAST


  KLABU ya Simba imemtambulisha rasmi beki Muivory Coast, Mohamed Outtara kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao.
  Ouattara, mwenye umri wa miaka 23, anajiunga na Simba akitokea klabu ya Al-Hilal Omdurman ya Sudan aliyojiunga nayo mwaka  2020.

  Outtarra anakuwa mchezaji mpya wa sita Simba baada ya beki, Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar, mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza iliyoshuka Daraja, kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union, mshambuliaji Mzambia,winga Mghana, Augustine Okrah kutoka klabu ya Asante Kotoko ya kwao na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMTAMBULISHA BEKI WA KATI MUIVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top