// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAKELELE ALIYEINUSURU SIMBA KUSHUKA DARAJA 1988 AFARIKI DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAKELELE ALIYEINUSURU SIMBA KUSHUKA DARAJA 1988 AFARIKI DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, July 03, 2022

  MAKELELE ALIYEINUSURU SIMBA KUSHUKA DARAJA 1988 AFARIKI DUNIA

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba SC, John Makelele ‘Zig Zag’ (pichani kushoto) amefariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili akiwa ana umri wa miaka 61.
  Kwa mujibu wa mke wa marehemu Salome, marehemu ameacha watoto watano ambao ni Happy (42), Esther (38), Jastaz (32), Francis (29) na Elizabeth (22).
  Salome amesema mazishi yatafanyika Jumanne nyumbani kwao, kijiji cha Mtakuja huko Moshi mkaoni Kilimanjaro. 
  Makelele ambaye pia amcheza timu ya taifa, alihamishiwa Muhimbili kwa matibabu wiki iliyopita akitokea hospitali ya Arusha baada ya hali yake kubadilika nyumbani kwake Manyara, alipokuwa anaishi na familia yake kufuatia kustaafu kazi benki ya CRDB.
  Enzi za uhai wake, Makelele atakumbukwa zaidi baada ya kufunga bao la pili dakika ya 58 akimchambua kipa Sahau Kambi, marehemu pia Julai 23, mwaka 1988, Simba ikishinda 2-1 dhidi ya Yanga na kunusurika kushuka Daraja. 
  Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Edward Chumila, marehemu pia dakika ya 21, wakati la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Issa Athumani dk. 36.
  Mungu ampumzishe kwa amani marehemu John Makelele. Amin.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKELELE ALIYEINUSURU SIMBA KUSHUKA DARAJA 1988 AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top