• HABARI MPYA

  Tuesday, July 19, 2022

  YANGA YAWATEMA CHICO USHINDI NA YACOUBA SOGNE


  KLABU ya Yanga imeachana na wachezaji wawili wa kigeni, kiungo mshambuliaji Chico Ushindi aliyekuwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne ili kubaki na wachezaji 12 kwa mujibu wa kanuni.
  Wachezaji wa kigeni wanaobaki Yanga sasa ni beki Mkongo, Lomalisa Mutambala kutoka Sagrada Esperança ya Angola, viungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki kutoka ASEC Mimosa ya Ivory Coast, Mrundi, Gael Bigiriamana kutoka Glentoran ya Ireland Kaskazini, winga Mghana, Bernard Morrison kutoka Simba na mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
  Hao wanaungana na waliokuwepo tangu msimu uliopita, kipa wa kimataifa wa Mali, Djigui Diarra Wakongo, beki Djuma Shabani, viungo Yanick Bangala, Jesus Moloko, Mganda Khalid Aucho na weashambuliaji Wakongo pia, Heritier Makambo na Fiston Mayele kufanya idadi ya wachezaji 12 wa kigeni.
  Kikosi kizima cha Yanga kinatarajiwa kuingia kambini keshokutwa huko Avic Town, eneo la Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya.
  Yanga SC watazindua katika kikosi chao kipya katika kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 6, kabla ya kumenyana na watani wa jadi, Simba SC katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAWATEMA CHICO USHINDI NA YACOUBA SOGNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top