• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2022

  AZAM FC SASA YASAJILI KIUNGO MNIGERIA


  KLABU ya Azam FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya kumtambulisha kiungo mkabaji, Isah Ndala kutoka Plateau United ya kwao, Nigeria aliyesaini mkataba wa miaka miwili.
  Usajili wa Ndala, moja kati ya vya kusifika nchini Nigeria umekamilishwa na Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa akishirikiana na Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na anakuwa mchezaji mpya wa tatu wa kigeni, baada ya viungo wawili washambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Junior na Tape Edinho.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC SASA YASAJILI KIUNGO MNIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top