• HABARI MPYA

  Sunday, July 17, 2022

  AZAM FC WATWAA UBINGWA LIGI YA VIJANA U17

  TIMU ya vijana chini ya miaka 17 ya Azam FC imetwaa ubingwa wa ligi ya vijana wa umri huo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Karume jana.
  Azam FC waliingia kwenye mchezo huu wakihitaji sare tu ili kuwa mabingwa baada ya kujikusanyia alama 25 katika michezo 9 iliyokuwa imeshafanyika.
  Kwa hiyo katika mchezo huo wa 10, Sare tu ingetosha kuwahakikishia ubingwa lakini vijana hao wa Mohamed Badru hawakutaka kubahatisha kwani walicheza kwa nguvu na maarifa makubwa na kuutawala mchezo. 
  Dakika ya tano tu ya mchezo, Abdulkareem Kiswanya akaipatia Azam FC bao la kwanza akiungamisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo kutoka upande wa kushoto wa uwanja.
  Dakika ya 30 Azam FC wakapata penati iliyopigwa na Cyprian Kachwele lakini ikaokolewa na kipa wa Yanga.
  Hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-0 kwa faida ya Azam FC. 
  Kipindi cha pili Kachwele akarekebisha makosa yake ya kukosa penati na kufunga bao maridadi kwa mguu wa kushoto.
  Bao hilo likatosha kuihakikishia Azam FC ushindi katika mchezo ambao Azam FC waliutawala kwa kiasi kikubwa.
  Hadi inatawazwa mabingwa, Azam FC imebaki na michezo miwili mkononi, baada ya kucheza michezo 10, wakishinda 9 na kutoa sare mmoja.
  Wamefunga mabao 30 na kufungwa manne tu.
  Naye mshambuliaji wa Azam FC, Cyprian Kachwele, anaongoza mbio za ufungaji bora akiwa na mabao 14.


  Orodha ya mechi za Azam FC
  Julai 16, 2022
  Yanga 0-2 Azam FC 
  -Abdulkareem Kiswanya 5'
  -Cyprian Kachwele 67'
  Julai 9, 2022
  Azam FC 3-1 Green Warriors 
  -Cyprian Kachwele ⚽⚽
  -Ali Golo ⚽
  Julai 5, 2022
  JKT Tanzania 1-6 Azam FC 
  -Cyprian Kachwele manne ⚽⚽⚽⚽
  -David Chiwalanga moja ⚽
  -Daud Said ⚽
  Julai 3, 2022
  JMK Park 0-0 Azam FC 
  Juni 30, 2022
  Azam FC 4-0 Transit Camp 
  -Cyprian Kachwele ⚽⚽⚽
  -David Chiwalanga ⚽
  Juni 25, 2022
  Azam FC 4-1 KMC 
  -David Chiwalanga ⚽⚽
  -Cyprian Kachwele ⚽
  -Daud Said ⚽
  Juni 22, 2022
  Azam FC 3-0 African Sports
  -Mohamed Ismail ⚽⚽
  -David Chiwalanga ⚽
  Juni 18, 2022
  Azam FC 3-0 Magnet Youth 
  -Amos Nada ⚽
  -Daud Said ⚽
  -Cyprian Kachwele ⚽
  Juni 15, 2022
  Ruvu Shooting 1-2 Azam FC 
  -Amos Nada ⚽
  -Abdulkareem Kiswanya⚽
  Juni 11, 2022
  Azam FC 5-0 Cambiaso 
  -Daudi Said ⚽️⚽️ 
  -Cyprian Kachwele ⚽️⚽️
  -Arafat Masoud ⚽️
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WATWAA UBINGWA LIGI YA VIJANA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top