• HABARI MPYA

  Monday, July 04, 2022

  WAANZANIA KUCHEZESHA BURUNDI NA DJIBOUTI CHAN


  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua marefa wa Tanzania, Elly Sasii, Mohamed Mkono, Soud Lila na Ramadhan Kayoko kuchezesha mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baina ya Djibouti na Burundi.
  Katika mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Julai 29, mwaka huu, Kamisaa pia ni Mtanzania, Khalid Abdallah ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TFF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAANZANIA KUCHEZESHA BURUNDI NA DJIBOUTI CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top