• HABARI MPYA

  Sunday, July 24, 2022

  SAKHO APIGA MBILI, SIMBA YASHINDA 6-0 MISRI


  TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, Abo Hamad ya Misri katika mchezo wa kirafiki mjini Ismailia nchini Ismailia usiku wa Jumamosi.
  Mabao ya Simba yamefungwa na mshambuliaji mpya, Mzambia Moses Phiri, kiungo Jonas Mkude, mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere, winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho mawili na kiungo mkongwe Erasto Edward Nyoni.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili wa Simba chini ya kocha mpya, Mserbia Zoran Manojilovic ‘Maki’ katika kambi yake ya Misri kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kutoka sare ya 1-1 na Ismailia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKHO APIGA MBILI, SIMBA YASHINDA 6-0 MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top