• HABARI MPYA

  Saturday, July 02, 2022

  YANGA WAKAMILISHA NDOTO ZA KUKUSANYA MATAJI YOTE BARA


  VIGOGO, Yanga SC wametimiza malengo ya kutwaa mataji yote matatu ya Bara msimu huu.
  Hiyo ni baada ya kuifunga Coastal Union ya Tanga kwa penalti 4-1 kufuatia sare ya 3-3 ndani ya dakika 120 katika fainali tamu ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Sheik Amri Abeid Jijini Arusha. 
  Mabao yote ya Coastal leo yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ dakika za 11, 86 na 98 kutimiza jumla ya magoli tisa kwenye michuano hiyo msimu huu.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 57, mshambuliaji Mkongo Heritier Ebenezer Makambo dakika ya 82 na winga Dennis Nkane dakika ya 113.
  Waliofunga penalti za Yanga ni walinzi, Yannick Bangala, Dickson Job, Makambo na kiungo Mganda, Khalid Aucho, wakati kwa upande wa Coastal aliyefunga ni kiungo Mnigeria pekee, Victor Akpan huku ya Amani Kyata ikigonga nguzo kulia, kabla ya kipa Djigui Diarra kuokoa ya Rashid Chambo.
  Yanga wanakamilisha msimu na Medali tatu za Dhahabu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na ASFC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAKAMILISHA NDOTO ZA KUKUSANYA MATAJI YOTE BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top