• HABARI MPYA

  Wednesday, July 13, 2022

  PRISONS YAITOA JKT, YABAKI LIGI KUU 2022-2023


  TIMU ya Tanzania Prisons itaendelea kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuitoa JKT Tanzania katika mchujo wa kuwania kucheza ligi hiyo.
  Prisons imelazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, hivyo kuwatupa nje JKT kwa ushindi wa jumla 2-1 kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Katika mchezo wa leo, JKT walitangulia kwa bao la penalti la Edward Songo dakika ya 36, kabla ya Benjamin Asukile kuisawazishia Prisons dakika ya 69 na mchezo wa kwanza bao pekee lilifungwa na Oscar Paul dakika ya 38 Uwanja wa Meja Isamuhyo.
  Sasa Prisons inabaki Ligi Kuu na JKT itaendelea kucheza Championship.
  Ikumbukwe Prisons imeingia kwenye mechi hii ya mchujo wa kuwania kucheza Ligi Kuu baada ya kutolewa na Mtibwa Sugar katika mchujo wa awali uliohusisha timu za Ligi Kuu, wakati JKT imetoka Championship ambako iliitoa KITAYOSCE.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAITOA JKT, YABAKI LIGI KUU 2022-2023 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top