• HABARI MPYA

  Thursday, July 14, 2022

  AZAM FC NAYO YASHUSHA NYOTA KUTOKA GHANA


  KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo mshambuliaji, Mghana James Akaminko kutoka Great Olympic ya kwao, Accrah.
  Akaminko, 26, ambaye ni mmoja wa viungo wabunifu kwenye Ligi Kuu ya Ghana, amesaini mkataba mbele mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
  Kiungo huyo nyota, aliyewahi kucheza soka la kulipwa nchini Tunisia katika timu ya US Tataouine, amepita pia kwa vigogo wa Ghana, Ashanti Gold na Medeama.
  Mbali na kucheza eneo la ushambuliaji, pia anao uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, na anakuja kuongeza nguvu katika eneo la kiungo kuelekea msimu ujao.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC NAYO YASHUSHA NYOTA KUTOKA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top