• HABARI MPYA

  Tuesday, July 12, 2022

  MSUVA AIBWAGA WYDAD FIFA, KULIPWA SH. BILIONI 1.6


  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiagiza Wydad Athletic ya Morocco kumlipa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva zaidi ya Dola za Kimarekani 700,000 (Tsh. zaidi ya bilioni 1.6).
  Hatua hiyo inafuatia Msuva kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya mabingwa hao wa Afrika.
  Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake Desemba mwaka jana kutokana na kuidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AIBWAGA WYDAD FIFA, KULIPWA SH. BILIONI 1.6 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top