• HABARI MPYA

    Friday, July 22, 2022

    MANE MWANASOKA BORA WA AFRIKA TENA

    NYOTA aliyejiunga na Bayern Munich akitokea Liverpool, Sadio Mane ameshinda tena Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mbele ya Msenegal mwenzake, kipa Edouard Mendy wa Chelsea na Mohamed Salah wa Misri na Liverpool.
    Ulikuwa usiku mzuri, baada ya Wasenegal wengine kubeba tuzo, Aliou Cisse akichukuwa ya Kocha Bora wa Mwaka, kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho akibeba Tuzo yaBao Bora la Mwaka na Pape Matar Sarr wa Tottenham Hotspur akiondoka na ya Mwanasoka Bora Chipukizi.
    Katika sherehe za utoaji wa Tuzo hizo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa Alhamisi mjini Rabat nchini Morocco, washindi wengine wa tuzo za CAF mwaka huu ni Asisat Oshoala wa Nigeria aliyebeba kwa mara ya tano ya rekodi Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike.
    Aisha, Senegal imeshinda tuzo ya timu Bora ya Taifa na Wydad Athletic ikibeba Tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume na Mamelodi Sundowns Klabu Bora ya Wanawake.
    WASHINDI WOTE TUZO ZA CAF
    BAO BORA LA MWAKA
    Pape Ousmane Sakho (Senegal & Simba)
    MWANASOKA BORA WA MWAKA WA KIUME
    Sadio Mane (Senegal and Bayern Munich)
    MWANASOKA BORA WA KIKE
    Asisat Oshoala (Nigeria and FC Barcelona)
    MCHEZAJI BORA WA KIKE WA KLABU
    Evelyn Badu (Ghana & Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)
    MCHEZAJI BORA WA KIUME WA KLABU
    Mohamed El Shenawy (Egypt & Al Ahly)
    MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIKE
    Evelyn Badu (Ghana & Sekondi Hasaacas Ladies/Alvaldsnes)
    MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA KIUME
    Pape Matar Sarr (Senegal and Tottenham Hotspur)
    KOCHA BORA WA MWAKA MWANAMKE
    Desiree Ellis (Afrika Kusini)
    KOCHA BORA WA MWAKA MWANAUME
    Aliou Cisse (Senegal)
    KLABU BORA YA MWAKA YA WANAWAKE
    Mamelodi Sundowns (South Africa)
    KLABU BORA YA MWAKA YA WANAUME
    Wydad Athletic Club (Morocco)
    TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME
    Senegal
    TIMU BORA YA TAIFA YA WANAUME
    Itapatikana baada ya Fainali ya Afrika za Wanawake zinazoendelea Morocco
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANE MWANASOKA BORA WA AFRIKA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top